Thursday, September 13, 2012

‘AUNTY EZEKIEL’ AWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE BAADA YA PICHA ZAKE ZA KUMDHALILISHA KUTANDA KWENYE MITANDAO…!!!


MSANII wa filamu bongo ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni, Aunty Ezekiel, amewaomba radhi mashabiki wake baada ya picha zake zinazomuonesha umbo lake la ndani kusambaa kwenye mitandao, huku akidai kuwa alipigwa picha hizo akiwa amelewa sana.

Picha za msanii huyo zimechukua sura mpya kwenye mitandao mingi ya kijamii, ambapo picha hizo zinataka kufanana na zile za mwanadada nyota wa video za wasanii wa bongo Agnes ambazo bado zinapatikana kwenye mitandao hiyo ya kijamii.

Hata hivyo baada ya kusamba kwa picha hizo mtandao wa DarTalk, ulitaka kujua ni kitu gani kilichosababisha hadi kupigwa kwa picha hizo huku nguo aliyokuwa amevaa ikiwa haina heshima mbele za watu, alidai kuwa haikuwa akili yake kwani alikuwa amelewa kiasi kwamba hakuna alichokuwa anakijua siku hiyo ya tukio mjini Tanga.

Msanii huyo alidai anaamini tukio hilo limetokea na hana budi kukaa kimya au kujiteteta lakini kikubwa anawaomba radhi wale walioziona picha hizo kwani yenye ni mwanadamu hajakamilika.

“Nimeziona kwa kweli ni picha ambazo zinaonesha umbo langu lakini nachoweza kusema kwa sasa ni kwamba wanaomba msamaha mashabiki wangu wote kwani kilichotokea ni kwa sababu ya pombe na nimejifunza kutokana na makosa,” alisema Aunty.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...