Wednesday, November 14, 2012

DIAMOND APATA AJALI

KILICHOSABABISHA AJALI YANGU NI HIKI HAPA....

Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.
Baada ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo jumamosi iliyopita.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale.(HAYA YOTE NI MAELEZO YA DIAMOND PLATNUMS)
Hii ni pikipiki ambayo ni chanzo cha ajali.....

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...