Wednesday, November 28, 2012

UPDATE ZA MSIBA WA SHARO MILIONEA: R.I.P SHARO


UPdate za msiba wa Sharo Milionea: Marehemu Sharo Milionea anatarajiwa kuzikwa leo saa 7 mchana huu kijijini kwao muheza Tanga karibu na nyumba yao ndipo lilipochimbwa kaburi.

Dada zake marehemu wasema alikuwa anaihudumia familia yake kwa kila kitu na wamesikitika sana maana ndiye alikuwa mtoto wa kiume pekee katika familia yao.

Pia hali ya Mzee majuto yatengemaa na anahudhuria msiba.

Viongozi wa serikali, wasanii wa filamu na muziki na wanakijiji wajitokeza kwa wingi katika msiba, vilio na majonzi vyatawala na sehemu kujaa hadi wengine kukosa sehemu ya kukaa.

Aliyekuwa Meneja wa marehemu Bw.HK ndio anaongoza ratiba ya mazishi na pia Bw.Jackson Mbwambo waliyefanya naye kazi ya Airtel asema wamepoteza mtu muhimu sana.





1 comment:

Dinewithme said...

May his soul rest in peace.
http://clothes-lovers.blogspot.com

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...