Monday, January 28, 2013

UPDATE KUHUSU LULU (ELIZABETH MICHAEL) KUACHIWA KWAKE KWA DHAMANA NA MASHARTI ALIYOPEWAMahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.

Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.

Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho ili Msajili wa Mahakama Kuu (hakuwepo) aweze kupitia nyaraka za wadhamini

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...