Sunday, April 13, 2014

MAJANGA MENGINE ARUSHA : BOMU LASADIKIWA KUJERUHI

Watu kadhaa wamejeruhiwa leo Aprili 13, 2014 na kitu kilichosadikiwa ni bomu la kurushwa kwa mkono lililolipua bar maarufu jijini Arusha ijulikanayo kwa jina la Arusha Night Park (Matako Bar) iliyopo eneo la Mianzini.
Kwa mujibu wa habari ilizozifikia chumba chetu cha habari zinasema kuwa kitu hicho kilichosadikiwa ni bomu kimelipuka kimesababisha uharibifu wa mali ikiwemo kuwajeruhi watu kadhaa.
"Mmoja ya mashuhuda ambaye ameongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu amesema tukio hili limetokea saa moja lililopita, ambapo kulikuwa na watu wengi waliokuw wakiangalia mpira.
Mpaka sasa polisi wameshafika eneo la tukio

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...