Monday, August 4, 2014

ALI KIBA: LULU ANAFAA KUWA MKE

Stori: Erick Evarist na Sifael Paul
HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba ndani ya ofisi za Global.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza mbele ya kinasa sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya kihistoria Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.


AMMWAGIA SIFA
Kiba alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).

Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akiwa na Ali Kiba.
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo hakuyatilia maanani. 
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?

Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke.
Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa?
Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.

ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na kujamiiana).
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.

'Kanumba The Great' enzi za uhai wake.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA 
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.

“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.

KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.

KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.

“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu  wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.

“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na mapaparazi wetu ili  azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake muda mwingi iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea kumtafuta ili afunguke).

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...