Monday, April 14, 2014
Sunday, April 13, 2014
BEDROOM EYES: RIHANNA
Rihanna
on the MTV Movie Awards red carpet
Rihanna as usual looked very sultry in a white
satin Ulyana Sergeenko dressing gown over a matching bustier
MAJANGA MENGINE ARUSHA : BOMU LASADIKIWA KUJERUHI
Watu kadhaa wamejeruhiwa leo Aprili 13, 2014 na kitu kilichosadikiwa ni bomu la kurushwa kwa mkono lililolipua bar maarufu jijini Arusha ijulikanayo kwa jina la Arusha Night Park (Matako Bar) iliyopo eneo la Mianzini.
Kwa mujibu wa habari ilizozifikia chumba chetu cha habari zinasema kuwa kitu hicho kilichosadikiwa ni bomu kimelipuka kimesababisha uharibifu wa mali ikiwemo kuwajeruhi watu kadhaa.
"Mmoja ya mashuhuda ambaye ameongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu amesema tukio hili limetokea saa moja lililopita, ambapo kulikuwa na watu wengi waliokuw wakiangalia mpira.
Mpaka sasa polisi wameshafika eneo la tukio
REST IN PEACE MUHIDIN MAALIM GURUMO
Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo amefariki alasiri hii katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Habari zilizofikia dawati letu zinasema kuwa mzee huyo amefariki kutokana na maradhi ambayo yalimsumbua kwa muda mrefu:
Septemba 10, 2012: Mwimbaji huyo Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma alifanikiwa kupanda tena jukwaani kukonga mashabiki wa bendi hiyo baada ya afya yake kulega lega kutokana kusumbuliwa na Maradhi.
Novemba 22, 2013: GWIJI wa muziki wa dansi mstaafu Muhidin Maalim Gurumo aliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mwimbaji huyo mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo.
Subscribe to:
Posts (Atom)