Watoto wawili Walifungua njia kwa kumwaga maua na show ya kupendeza
Madada na Makaka tukafuata kwa Show Maalumu
Bibi Harusi mratajiwa Veronica Stima akiwa amesindikiza na kaka yake John Stima kuingia katika ukumbi kwa ajili ya sherehe ya kumuaga (Send Off) iliyofanyika Student Centre, Tabora. Ambapo Harusi yake ni Jumamosi Septemba 22, 2012.
Tulifuata kwa show ya pamoja na Bibi harusi mtarajiwa
Baba na mama yake mzazi Veronica Stima (kutoka kulia) wakicheza wimbo wa kabila la Kifipa.
Wakwe wa bibi harusi mtarajiwa wakiingia ukumbini kwa madaha.
Bi Harusi mtarajiwa Veronica Stima akiwa na kaka na dada zake waliomsindikiza katika sherehe yake ya send off iliyofanyika ukumbi wa Student Centre, Tabora.
Bibi Harusi Mtarajiwa Veronica Stima akimlisha mtarajiwa wake Bw. Allen Mnene
Wachaga nao hawakuwa nyuma kuonyesha umoja wao na ule wimbo wao wa kushikana mikono.
Bwana harusi mtarajiwa Allen na mkewe mtarajiwa Veronica Stima wakienda mbele kwa ajili ya utambulisho.
...akilishwa keki na mtarajiwa wake
Bibi harusi mtarajiwa akiaga wazazi wake, kujitayarisha kuungana na mwenzake
...hapa bibi harusi mtarajiwa alikuwa akitoa keki kwa mama mkwe wake mtarajiwa huku kaka yake akiwa amemsindikiza.
Mzee Prosper Stima ambaye ni baba wa bibi harusi mtarajiwa akitoa machache.
Mama Catherine Stima ambaye ni mama mazazi wa bibi harusi nae alipata wasaa wa kutoa machache kwa mwanae.
Kaka mkubwa John Stima akiongea machache kabla ya kumkabidhi dada yake kwa shemeji zake. Alisema, 'Nawakabidhi dada yangu mpendwa, hana hata doa... nawaombeni msije mkanyanyasa'.
...mara baada ya kuongea machache kaka mkubwa alikabidhiwa begi la nguo za bibi harusi, tayari kwa maandalizi ya harusi.
Aha... Bwana na Bibi Cathbert Angelo nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Bibi harusi mratajiwa (wapili kutoka kulia) akiwa na dada zake.
Muda wa kupata show ulifika na mambo yalikuwa kama unavyoona mwenyewe....tulibadili tukavaa viatu maalumu vya show
Picha ya kumbu kumbu kwa wake na watoto wao. Nguo zote za shughuli hiyo zimedizainiwa na na kushonwa na mwanamitindo Manju Msita
No comments:
Post a Comment