KAMA kuna kitu kinakukwaza ndani ya moyo wako, siku zote ukikaa nacho kitazidi kukuumiza lakini ukiamua kumtafuta mtu ambaye umeshibana naye na kumsimulia, moja kwa moja utakuwa umeutua mzigo!
Hicho ndicho amekifanya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kwa kuweka kweupe chanzo cha ugomvi wake na staa mwenzake, Kajala Masanja huku akijuta kumlipia mwanadada huyo zile Sh. milioni 13 za faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza na Ijumaa katika exclusive interview Jumanne iliyopita, Wema ambaye pia ni staa mkubwa wa sinema za Kibongo alisema kuwa kuna mambo mazito ambayo yamesababisha yeye kuingia kwenye gogoro kubwa na Kajala.Wema au Beautiful Onyinye alisema kwamba mambo hayo ndiyo yamemsababishia maumivu ya moyo na kutokwa machozi kila wakati.
“Leo (anataja jina la mwandishi), ngoja nikuelezee kila kitu kinachohusiana na mimi na Kajala juu ya tofauti zetu.“Naamini baada ya kusimulia kisa na mkasa nitakuwa nimeutua huu mzigo mkubwa nilionao ndani ya moyo wangu.
“Baada ya hapo sitapenda tena kuzungumzia ishu inayonihusu mimi na Kajala,” alianza kufunguka Wema.
UZINDUZI WA KIGODORO
Katika maelezo yake, cha kwanza, Wema ni uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo yeye
alisema kuwa alianza kuyaamini yale yaliyokuwa yakisemwa na watu kuhusiana na Kajala.
Wema alisema kabla ya tukio, akiwa saluni akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi huo, ghafla Kajala alimharibia ‘mudi’. “Unajua ile Saluni ya (anataja jina la saluni) pale Kinondoni, ina sehemu mbili, juu na chini, sasa mimi nilikuwa juu na Aunt (Ezekiel) tunatengeneza nywele.
“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele, nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno yalishaanza kuwa mimi na Kajala tuna bifu, nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye.
“Kweli
nilipiga makelele ya furaha nilivyomuona K, nikawa nakimbia kwenda kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema nooo...Wema usinikumbatie na kuanza kutoa maneno ya dharau eti nitamchafua.
“Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi, basi huwezi kuamini, nilishindwa kujizuia nikajikuta namtukana, sikumbakisha.
“Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe, huwezi amini hali ya hewa iliharibika ghafla kwani sikuwa na mudi tena,” alitiririka Wema.
SAFARI YA ARUSHA KATIKA SHOO YA MIRROW
Wema alisema kuwa baada ya kutofautiana pale saluni, hakuwa na kinyongo, safari ya Arusha ilipofika walikwenda kumsapoti msanii wao wa Bongo Fleva anayesimamiwa na Kampuni ya Endles Fame Production.
Wakiwa njiani, kwa mujibu wa Wema, yeye alikuwa hana fedha taslimu za kutosha
zaidi ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti hivyo alimwambia Kajala ampe shilingi laki tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani pamoja na matumizi madogomadogo.
Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.
Aliendelea kutoa ya moyoni: “Tulipofika Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue fedha alizokuwa nazo akamuwekee benki kwa sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa eti nilijishaua kuandaa shoo nikitegemea fedha zake.
“Wakati K anazungumza hivyo kulikuwa na watu watatu, mimi sina hili wala lile nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni, wamekwenda wapi?
“Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu themanini, kiukweli iliniuma sana, Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa bali alinikopesha?
“Nilijiuliza amesahau mimi nilitoa Sh. milioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka saba? Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare, viatu sare, mapochi sare, ninachokula na kunywa mimi ndicho hichohicho.
“Siku zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu nilikuwa ni mimi, leo laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima ananitangazia kwa watu (anataja jina la mwandishi)?
“Iliniuma sana basi palepale, nikaenda benki nikatoa Sh. milioni mbili, nikamlipa fedha zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote kinachoendelea kwani ningefanya chochote ningeharibu shoo na isingekuwa na maana yoyote ya sisi kwenda Arusha.”
WAREJEA DAR, MAANDALIZI YA FILAMU YAKE YAANZA
Wema alisema waliporejea Dar, alimwambia Kajala kuwa kuna mtu aliyekuwa amempa stori hivyo alimuomba wafanye filamu wawili.
Alisema kwamba Kajala alikubali na kusema kuwa atachangia Sh. milioni tano katika bajeti ya filamu hiyo.Baada ya kusikia hivyo, Wema alisema alifarijika, alipokwenda kumweleza ‘bebi’ wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, naye Diamond akasema atatoa Sh. milioni tano hivyo jumla itakuwa Sh. milioni kumi ikapita bajeti iliyokuwa imepangwa ya Sh.milioni nane.
Anaendelea: “Tukiwa katika maandalizi ya mwisho tuanze ku-shoot, K alinipigia simu akaniambia hawezi ku-shoot kwani alikuwa na safari ya kwenda China labda wa-shoot vipande vyake, nikamwambia basi aende akirudi tutatengeneza nyingine.
“Baada ya kuona hivyo ndipo nikamchukua Aunt tutengeneze filamu. K alipoona nimemchukua Aunt, akanipigia simu na kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza mbona mwenzangu amesahau ghafla wema wangu niliomtendea au kwa kuwa tangu aanze vijisafari vyake vya kwenda China anapata.
Habari kwa hisani ya Global Publisher.